Klabu ya Fc Bayern Munich inafikiria kumrudisha golikipa wake aliyeenda kwa mkopo kwenye klabu ya As Monaco Alexander Nubel kama mbadala wa Manuel Neuer.

Golikipa Alexander Nubel ambaye anacheza kwa mkopo kwenye klabu ya As Monaco ya nchini Ufaransa anafikiriwa kama mbadala sahihi wa golikipa namba moja wa klabu hiyo ambaye hatakuepo msimu mzima uliobakia kutokana na majeraha.bayern munichManuel Neuer amefanyiwa upasuaji kwenye mguu wake na kuwaacha mabingwa hao wa Ujerumani kwenye wakati mgumu wa kutafuta mbadala wa golikipa huyo, Lakini pia golikipa namba mbili wa klabu hiyo Sven Ulreich yupo kwenye mipango ya klabu hiyo.

Mkurugenzi wa klabu hiyo Salihamidzic amesema wanahitaji kutafuta mbadala sahihi wa Manuel Neuer kwa kipindi hichi kifupi, Na Alexander Nubel anaweza kua mbadala sahihi kwa kipindi hichi lakini amesema klabu ya As Monaco ndo wenye kauli ya mwisho.bayern munichKlabu ya Bayern Munich pia inahusishwa na golikipa anayecheza kwenye klabu ya Borussia Monchengladbach raia kutokana Uswisi Yann Sommer, Huku wakijitoa kwenye mbio za kumuwania kipa wa timu ya taifa ya Croatia Dominik Livakovic anayekipa katika klabu ya Dinamo Zageb ya nchini Croatia.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa