Klabu ya Fc Bayern Munich imeendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga baada ya kupata ushindi wa magoli matatu kwa mawili dhidi ya klabu ya Hertha Berlin.
Klabu hiyo ambayo imekua kwenye mfululizo wa matokeo bora kipindi cha hivi karibuni baada ya kua nje ya kiwango kwa kipindi fulani, Lakini kwasasa timu hiyo chini ya mwalimu Julien Nagelsman imerudisha ubora wake kwa kiwango kikubwa.
Mshambualiaji wa klabu hiyo raia wa Cameroon Choup Moting ambaye amekua kwenye kiwango bora sana ambaye amefunga kwenye michezo takribani minne mfululizo, Na leo pia amefanikiwa kufunga mabao mawili ati ya mabao matatu waliyofunga Bayern Munich na kuwapa alama tatu ugenini huku Jamal Musiala akifunga bao moja.
Baada ya Bayern Munich kushinda na kuendelea kujikita kileleni lakini pia Borussia Dortmund wamepata ushindi wa mabao matatu kwa bila nyumbani dhidi ya Bochum, Huku klabu ya Rb Leipzig nao wakipata alama tatu huku mshambuliaji wao hatari Christopher Nkunku akifunga mabao mawili.

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.
BONYEZA HAPA

