Klabu ya Bayern Munich wamepangwa dhidi ya Mainz katika hatua ya 16 bora ya kombe la DFB-Pokal, huku Borussia Dortmund wakimenyana na Bochum.
Bayern ambao ndio washindi mara nyingi wa kombe hili, mara 20 iliwashinda Viktoria Koln kwa kuwatandika mabao 5-0, na kuwafunga Augsburg kwa mabao 5-2 na kufika raundi ya tatu kwa mara ya kwanza katika misimu mitatu.
Kikosi cha Julian Nagelsmann sasa kinakabiliwa na safari ngumu kuelekea Mainz, ambao wako katika nafasi ya sita kwenye Bundesliga na wamewashinda Bayern katika mechi zao mbili zilizopita kwenye ardhi ya nyumbani.
Lakini kwa upande wa Dortmund wao ambao ni wapizani wao wamepangwa dhidi ya Bochum huku safari ya kwenda kuwakabili ikiwasubiri wakati mechi zitakapochezwa mwishoni mwa Januari.
Mabingwa watetezi RB Leipzig watakuwa wenyeji wa Hoffenheim ambao wapo nafasi ya saba kwenye msimamo na wamepishana pointi mbili, wakati huo huo vinara wa Bundesliga Union Berlin watakuwa nyumbani kumenyana na Wolfsburg.
Kwingineko, Sandhausen wamepangwa dhidi ya Freiburg, Stuttgart watamenyana na Paderborn, Eintracht Frankfurt mwenyeji Darmstadt na Nurnberg watakutana na Fortuna Dusseldorf.