Ligi kuu ya NBC kuendelea hii leo ambapo walima alizeti wa Singida, Singida Big Stars watawaalika Ihefu kwenye mchezo wao wa raundi ya 8 huku timu zote zikitoka kupata ushindi mechi zao zilizopita.
Singida walishinda dhidi ya Kagera kwa mabao mawili kwa 1 na kupata pointi tatu muhimu. Walima alizeti hao wamepanda ligi kuu msimu huu huku wakichukua wachezaji wazoefu wa ligi wakiwemo Meddie Kagere, Amis Tambwe, Metacha Mnata na wengi wengi ambao wameongeza kitu kwenye timu hiyo.
Wakati Ihefu wao walipanda daraja, msimu juzi, wakashuka na sasa wamepanda tena ambapo wameanza vibaya mno ligi baada ya kuwa na matokeo mabovu. Katika mechi saba amabazo wamecheza ndio kwanza wamepata ushindi mechi wa kwanza mechi yao iliyopita dhidi ya Dodoma.
Singida ambayo ipo chini ya mwalimu Pluijm ipo nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC huku akishinda mechi 3 kapata sare mbili na amepoteza michezo miwili mpaka sasa, pia amejikusanyia alama 11.
Kwa upande wa Ihefu yeye kacheza michezo 7, kashinda mchezo mmoja tuu, amepata sare 2, kapoteza michezo minne, na ana pointi 5 mpaka sasa na anashikilia nafasi ya 14 ambayo sio nzuri kwani yupo sawa pointi na kibonde wa Ligi na kama ataendelea na mwenendo huo anaweza akashuka daraja.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa katika uwanja wa Liti huko Singida majira ya saa kumi kamili ambapo nafasi kubwa ya ushindi kwenye Meridianbet wakipewa walima alizeti wakiwa na ODDS ya 1.65, Sare imepewa ODDS ya 2.94 na Ihefu amepewa ODDS ya 5.09.