Kocha mkuu wa FC Barcelona Xavi Hernandez amemsifu mchezaji wake Ousmane Dembele baada ya kung’ara hapo jana katika ushindi wao mkubwa wa Laliga wa mabao 4-0 dhidi ya Athletic Bilbao kwenye uwanja wa Camp Nou.
Barca walirudi nyuma kwa pointi tatu nyuma wiki iliyopita baada ya kubamizwa vibaya na wapinzani wao wakuu wa Laliga Real Madrid. Barca mabao yao yalifungwa na Robero Lewandowski, Sergio Roberto, Ferran Torres na Ousmane Dembele, huku Dembele alihusika na mabao yote manne hapo jana.
Hivyo basi kwa kuhusika na mabao hayo yote manne yanamfanya Dembele kuwa ni mara yake ya kwanza kuhusika kwenye mabao yote kwenye mchezo mmoja akiwa na Barcelona, ikiwa ni mechi yake ya 165 akiwa na Wacatalunya hao.
Dembele amefikisha pasi tano za mabao katika LaLiga kwenye mashindano msimu huu, na Xavi amemtaja mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kama mleta mabadiliko kwenye kikosi hicho kufuatia ushindi wa wa hapo jana. Xavi amesema kuwa;
“Alielewa kila kitu vizuri. Yuko hapa kuleta mabadiliko na ana uwezo wa kufanya mambo haya.”
Barcelona walifunga mabao hayo matatu ndani ya dakika 22 na kocha huyo amesema kuwa alidhani ulikuwa mchezo wa nguvu na walielewa kwamba wangewawekea shinikizo kubwa.
“Tulitoka katika wiki ngumu baada ya kupoteza dhidi ya Madrid, lakini tumejirekebisha kwa michezo miwili mizuri na tunaendelea kupigania nafasi za juu hapa,” Busquets alisema.
Anasema kuwa walitoka kwa nguvu sana na kwasababu walijua kuwa ni timu yenye nguvu sana na walitaka kuendana na kiwango hicho kwani walikuwa na dakika kumi za mafanikio mkubwa mbele ya lango na hivyo ilifanya iwe rahisi kwao kushinda mechi.
Mechi inayofuata kwa Barca ni ya Ligi ya Mabingwa ambapo watakuwa wakimenyana dhidi ya Bayern Munich siku ya Jumatano ambaye ndiye kinara wa kundi hilo, huku wakihitaji ushindi huo kwa hali na mali ili waweze kujihakikishia nafasi ya kufuzu hatua inayofuata.