Liverpool Imeripotiwa Kumtaka Moukoko

Inaripotiwa kuwa klabu ya Liverpool wanaongoza katika kinyang’anyiro cha kuwania saini ya kinda Borussia Dortmund Youssoufa Moukoko ambaye ni raia wa Ujerumani na ana miaka 18 mpaka sasa.

 

Liverpool Imeripotiwa Kumtaka Moukoko

Mshambuliaji huyo tayari ni mchezaji ambaye amekuwa anaanza mara nyingi katika kikosi cha kwanza cha Dortmund na ameanza kampeni akiwa katika kiwango kizuri, akifunga mara nne katika mechi 10 za Bundesliga.

Moukoko ameshiriki katika michezo 16 katika mashindano yote na anaonekana kuwa nyota wa hivi punde zaidi kutoka kwenye mstari wa uzalishaji wa Dortmund ambaye anaongeza kitu kwenye klabu hiyo.

Liverpool Imeripotiwa Kumtaka Moukoko

Kiwango cha mchezaji huyo ambaye anacheza katika timu ya Taifa ya Ujerumani chini ya miaka 21 tayari umevutia baadhi ya vilabu vikubwa barani Ulaya, huku Liverpool wakiwa mstari wa mbele kumuwania mchezaji huyo kulingana na jarida la Uhispania la Sport.

Jurgen Klopp amefurahishwa sana na uchezaji wa mchezaji huyo chipukizi katika klabu yake ya zamani na kumuona kama nyota wa siku zijazo wa safu yake ya ushambuliaji Anfield huku Darwin Nunez na Fabio Carvalho wakiwa tayari wameletwa hivi karibuni.

Moukoko anahitajika klabuni hapo kwaajili ya kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji huku Klopp akijiandaa kwa maisha bila ya kuwepo Mohamed Salah na Roberto Firmino, Lakini Dortmund bado hawajapata mustakabali wa kijana huyo amabye anatazamiwa kuwa huru mkatab wake utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu.

Liverpool Imeripotiwa Kumtaka Moukoko

 

Liverpool wanajua kuwa haitakuwa rahisi kuinasa saini ya mchezaji huyo huku vilabu vya Barcelona, Real Madrid na Paris Saint-Germain ambavyo pia vinasemekana kuwa vinamfuatilia kwa karibu kinda huyo.

Liverpool wanatarajia kumenyana dhidi ya Ajax siku ya Jumatano kwenye mchezo wa Klabu Bingwa baada ya kupoteza mchezo wa ligi hapo jana dhidi ya Nottingham Forest.

 

Acha ujumbe