Mexime: Tutapata pointi tatu mbele ya Simba

Kocha Mkuu wa kikosi cha Kagera Sugar, Mecky Mexime amesema kuwa kuelekea kwenye mchezo wao wa leo dhidi ya Simba watapata pointi tatu.

Mchezo huo utapigwa leo kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera saa 1:00 usiku.

Akizungumzia maandalizi yao, Mexime alisema “Tunatambua kwamba tunaenda kucheza na timu ambayo ipo vizuri ni mechi ngumu ambayo kidogo inaumiza kichwa.

Mexime: Tutapata pointi tatu mbele ya Simba

“Inabidi kocha utulie ili wachezaji waweze kupata ushindi, Simba na Yanga wala hazina ugenini wala nyumbani kwani wakija kwako ni nyumbani na ukienda kwao ni nyumbani.

“Sisi tunajua tunaenda kucheza na timu kubwa ina wachezaji wakubwa kwahiyo tumejiandaa vizuri, nawaomba mashabiki waje kuangalia mchezo mzuri na mimi naamini tutapata pointi tatu wala hilo hatuna shaka nalo.”

Acha ujumbe