Baada ya ushindi mnono hapo jana wa mabao 5-0 dhidi ya Geita Gold klabu ya Simba imesafiri hii leo kuelekea Bukoba ambapo siku ya Jumatano watamenyana dhidi ya Kagera Sugar.

 

Simba Yaanza Safari Kuelekea Bukoba Kuvaana na Kagera Sugar

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa saa 1:00 jioni katika uwanja wa Kaitaba huku Kagera Sugar wao wakitoka kupata sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Azam FC.

Ushindi huo wa jana ulimfanya Simba apande hadi nafasi ya pili ya msimamo akiwa na pointi zake 37 akiwa nyuma pointi 4 dhidi ya kinara wa Ligi Yanga ambaye ana pointi 41 mpaka sasa.

Simba Yaanza Safari Kuelekea Bukoba Kuvaana na Kagera Sugar

Wakati kwa upande wa Kagera Sugar baada ya kujivuia alam moja, anashikilia nafasi ya 6 akiwa na pointi zake 22, baada ya kushinda mechi zake 6, sare nne, na kupoteza mara sita.

Mechi ya mwisho kukutana kati yao Mnyama aliondoka na pointi zake tatu muhimu kwa kujifungia mabao 2-0. Hivyo Kagera anataka kulipiza kisasi kwa kutaka pointi tatu, lakini ataweza kwa kikosi cha Mgunda kinachoonekana chenye ubora?

Simba Yaanza Safari Kuelekea Bukoba Kuvaana na Kagera Sugar

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa