Klabu ya soka ya Simba imefanikiwa kupata ushindo mnono dhidi ya klabu ya Geita Gold katioka mchezo wao wa kwanza wa raundi ya pili wa wa ligi kuu ya NBC.

Wekundu wa Msimbazi wamefanikiwa kupata alama tatu muhimu katika dimba la ugenini baada ya kuichabanga klabu ya Geita Gold kwa jumla ya mabao matano kwa bila,Huku wakifanikiwa kurudi kwenye nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 37.simbaAlikua John Raphael Bocco aliewapatia wekundu wa msimbazi bao la kuongoza akipokea krosi tamu ya Shomari Kapombe, Kabla ya Clatous Chama kufunga bao la pili kabla ya timu hizo kwenda mapumziko na timu hiyo kwenda mapumziko wakiongoza mabao mawili kwa bila.

Klabu ya Simba iliingia kipindi cha pili wakiendelea kutafuta nafasi kufunga mabao huku wakichukua mchezo kwa kiwango kikubwa, Ambapo mchezaji Pape Ousmane Sakho alifanikiwa kuweka goli la tatu kimiani na bila kusubiri mchezaji huyo huyo aliongeza bao la nne la mchezo huo.simbaKlabu ya Simba wanafanikiwa kupata bao la tano kutoka kwa Kibu Dennis alietokea benchi na kuhitimisha karamu ya mabao katika mchezo huo, Klabu hiyo inakua nafasi ya pili lakini wakiendeleza rekodi yao ya kua timu iliofunga mabao mengi kwenye ligi hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa