Golikipa wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Julio Cesar amesema watu kutoka Brazil wanapaswa kushabikia timu ya taifa ya Ufaransa.

Golikipa huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil amesema watu wanaotokea nchi ya Brazil wanapaswa kuishabikia timu ya taifa ya Ufaransa katika mchezo wa fainali wa kombe la dunia kutokana na uhasimu uliopo baina yao na Argentina.julio cesarGwiji Julio Cesar anasema yeye anampenda Messi lakini kila Mbrazil anapaswa kushabikia timu ya taifa ya Ufaransa kwakua kama wao Brazil wangekua wanacheza fainali basi Waargentina wasingewaunga mkono na badala yake wangeshabikia wapinzani wao.

Timu ya taifa ya Argentina inacheza mchezo wake wa fainali leo dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa, Ambapo watu wengi duniani wanatamani kuona nyota wa timu hiyo Lionel Messi anabeba taji hilo kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya kwenye mpira wa miguu.julio cesarKumekua na upinzani mkali sana kati ya mataifa mawili ya Argentina pamoja na Brazil hivo hii inafanya mashabiki wengi pia kutoka nchi hizo kutokuungana mkono, Na hii ndo sababu Julio Cesar anaamini wao hawapaswi kuwaunga mkono Argentina.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa