Kiungo wa timu ya taifa ya Morocco na klabu ya Fiorentina inayoshiriki ligi kuu nchini Italia Sofyan Amrabat amepokea sifa tena kutoka kwa kiungo fundi wa Croatia Luca Modric.

Kiungo Sofyan Amrabat amekua na kiwango bora sana kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka huu akiitumikia timu ya taifa ya Morocco, Huku akiwa moja ya wanajeshi muhimu chini ya kocha Walid Regragui.amrabatSiku chache zilizopita katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa alipokea sifa kutoka kwa rais wa nchi ya Ufaransa na kumwambia kiungo huyo ni kiungo bora wa mashindano ya kombe la dunia.

Baada ya mchezo wa mshindi wa tatu jana kati ya timu ya taifa ya Morocco dhidi ya timu ya taifa ya Croatia, Kiungo Luca Modric alionekana na Amrabat baada ya mchezo kumalizika na inaelezwa pia Modric allikubali uwezo wa kiungo huyo na kumueleza yeye ni kiungo bora wa mashindano.amrabatKiungo Sofyan Amrabat amekua na michuano mizuri sana huku akiisaidia timu yake ya Morocco kufika busu fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza kabisa, Amekua akipokea sifa nyingi kutokana na ubora ambao ameonesha kwenye michuano hii.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa