Kocha wa klabu ya Juventus Massimiliano Allegri amekataa kuthibitisha kua kiungo wake Paul Pogba kwamba amerejea kutoka kwenye majeraha yaliokua yanamkabili.

Paul Pogba ambaye hajafanikiwa kucheza mchezo hata mmoja wa kiushindani na klabu ya Juventus tangu arejee klabuni hapo majira ya joto akitokea klabu ya Manchester United ya nchini Uingereza kutokana na majeraha yaliomuweka nje.allegriKiungo huyo alitarajiwa kurudi kwenye mchezo wa ligi kuu ya Italia mwezi Januari 13, Lakini taarifa zinaeleza tarehe hiyo imesogezwa mbele tena kwakua mchezaji huyo bado hajakua fiti kuanza kuitumikia klabu hiyo.

Kocha Allegri alizungumza kuhusu kurejea kwa kiungo huyo na kusema amekua hana mwendelezo mzuri kwenye mazoezi yake hivo siwezi kueleza ni lini atarejea, pia kocha huyo akisema huo ndo ukweli ambao waandishi wa habari wanapaswa kuusikia maana bila hivo watauliza swali hilohilo kila siku.allegriPia kocha Allegri ameongelea wachezaji wengine kwenye kikosi hicho kama Federico Chiesa ambae anasema ana shida ya misuli japo sio kubwa,Huku akisema beki wake Leonardo Bonucci hatakua nje kwa muda mrefu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa