Achraf Hakimi amepuuza uvumi kwamba alihusika katika ugomvi na Rais Gianni Infantino baada ya ripoti kupendekeza FIFA ilikuwa ikijaribu kuficha picha za tukio kati ya wawili hao.
Tukio hilo linadaiwa kutokea baada ya timu ya Morocco kufungwa mabao 2-1 na Croatia katika hatua ya mtoano ya kuwania nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Dunia, huku timu hiyo ya Afrika ikikosa kufurahishwa na kiwango cha mwamuzi wakati wa mchezo huo.
Inaaminika Hakimi alimkabili Infantino kuhusiana na maamuzi yaliyofanywa na mwamuzi wa Qatar Abdulrahman Al-Jassim wakati wa mchezo ambao uliisha 2-1 kwa Croatia baada ya bao maridadi la Mislav Orsic kufuatia magoli ya mapema kutoka kwa Josko Gvardiol na Achraf Dari.
Inasemekana Hakimi alitoka kwa hasira kuelekea kwa Infantino na ‘kupiga kelele usoni mwake’ kuhusu makosa yaliyofanywa na waamuzi katika dimba hilo.
Kulingana beIN Sports, inaaminika Hakimi alikuwa akizungumza na maafisa wa FIFA alipokutana na Infantino. Hapo ndipo alipomwendea kiongozi huyo wa Uswisi-Italia na maneno ya kuchagua kabla ya kuongozwa na wachezaji wenzake wa Morocco.
Shirikisho la soka duniani sasa limejaribu kupunguza kisa hicho, ambacho kinadaiwa kuwa kilitokea wakati rais wa FIFA Infantino alipokuwa akisubiri kukabidhi medali kwa wachezaji wa Croatia baada ya mchezo.
Hata hivyo, beki wa PSG Hakimi alisema kisa hicho kilikuzwa na ameomba msamaha kwa Infantino: “Hakuna kilichotokea. Nilikuwa na hasira baada ya kumalizika kwa mechi,” Hakimi aliwaambia waandishi wa habari, kupitia Arryadia TV. “Nilienda kuongea naye, na nikamuomba msamaha kwa maneno niliyomwambia. Ni rafiki yangu na ninamheshimu sana, kwa hiyo hakuna kilichotokea.”
Hakimi na wachezaji wenzake wa Morocco walikasirishwa baada ya maamuzi mawili kwenda kinyume nao katika nyakati muhimu wakati wa mchezo huo, na kuwaacha wakimaliza nafasi ya nne baada ya kutinga hatua ya kihistoria ya nusu fainali.