Matip Amsifu Konate Kuelekea Fainali ya Kombe la Dunia

Beki wa klabu ya Liverpool Joel Matip amemsifu mchezaji mwezake wa klabu hiyo Ibrahim Konate anayekipiga timu ya taifa ya Ufaransa kuelekea mchezo wa fainali leo kati ya Ufaransa dhidi ya Argentina.

Beki Ibrahim Konate ambaye ameshiriki michezo minne katika michuano ya kombe la dunia akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa, Huku akijizolea sifa katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Morocco ambapo alionesha kiwango kikubwa zaidi baada ya kuchukua nafasi ya beki wa Dayot Upamecano aliekua anaumwa.MatipJoel Matip ameongeza sifa ambazo amekua akipokea Ibrahi Konate baada ya kusema mchezaji huyo ni mdogo lakini tayari ameshaonesha ubora akiwa na kalbu ya Liverpool na sasa akifanya hivo na timu ya taifa ya Ufaransa.

beki Matip amesema inashangaza kwa mchezaji mdogo kama Konate anaweza kua bora katika maeneo yote akieleza kua beki huyo ana nguvu katika mpambano, kasi, na pia ni mtulivu akiwa na mpira na kumalizia beki ana kila kitu anachotakiwa kua anacho mlinzi.MatipIbrahim Konate mwenye miaka 23 ni miongoni mwa wachezaji waliokua wanaumwa siku za hivi karibuni katika kambi ya timu ya taifa ya Ufaransa, Lakini ripoti zilizotoka zinasema mchezaji huyo yupo fiti kwajili ya kucheza mchezo wa fainali dhidi ya timu ya taifa ya Argentina.

Beki Joel Matip pia anasema wachezaji wote wa Liverpool leo watakua wanampa ushirikiano mchezaji huyo, Kwakua ndo mchezaji pekee kutoka klabu ya Liverpool ambaye amebaki katika michuano ya kombe la dunia nchini Qatar.

Acha ujumbe