Allegri: Juventus Watumie Hasira ya Ligi ya Mabingwa Kama Motisha

Kocha wa klabu ya Juventus Massimiliano Allegri amewataka wachezaji wake kutumia hasira zao zote za kushindwa kwao kwenye Ligi ya Mabingwa kama motisha ya kufanikiwa kwenye Ligi ya Europa.

 

Allegri: Juventus Watumie Hasira ya Ligi ya Mabingwa Kama Motisha

Allegri alipokea kichapo cha 2-1 kutoka kwa wababe wa Ufaransa PSG, mjini Turini na kuifanya Juventus kuwa ni timu ya pili ya Italia kupoteza mechi 5 kati ya 6 za hatua ya makundi kwenye michuano hiyo, baada ya Roma kuonolewa kwenye miaka ya 2004-2005.

Massimiliano Allegri amewataka Juventus kutumia hasira ya kushindwa kwao kwa Ligi ya Mabingwa kama motisha ya kufanikiwa katika Ligi ya Europa.

Allegri: Juventus Watumie Hasira ya Ligi ya Mabingwa Kama Motisha

Kichapo cha 2-1 kutoka kwa Paris Saint-Germain mjini Turin kiliifanya Juve kuwa timu ya pili ya Italia kupoteza mechi tano kati ya sita za hatua ya makundi kwenye michuano hiyo, baada ya Roma mwaka wa 2004-05 – ingawa kuondolewa kwao tayari kumethibitishwa.

Katika Ligi ya Europa, Juve itachukuliwa kuwa miongoni mwa wanaopewa nafasi kubwa ya kusonga mbele na Allegri ameitaka timu yake kutumia hasira zao ili kuwapa matokeo bora zaidi katika mashindano hayo ya Europa ambapo timu kubwa pia zimeangukia huko akiwemo Barcelona.

Kocha huyo alishindwa kujizuia na akasema kuwa; “Tulicheza mchezo mzuri, ni aibu kwa matokeo, tupo kwenye Ligi ya Europa kuanzia kesho lazima tufungue ukurasa wa Ubingwa, lazima tuwe na hasira na mara moja tuanze kazi nzuri”

Allegri: Juventus Watumie Hasira ya Ligi ya Mabingwa Kama Motisha

Alisema kuwa pia kwa upande mwingine pia kuna sababu ya kuridhika kufika Ligi ya Europa lakini pia kwa upande mwiingine kuna hasira ya kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa. Bado Allegri ana hasira sana na wanapaswa kubeba hasira hiyo ndani yao katika michezo ijayo ya Europa.

Na pia furaha tuliyonayo ni kurejea kwa Federico Chiesa kutokana na jeraha alilolipata, na amekosekana tangu Januari, ingawa ahueni yake haitahakishwa huku mchezaji huyo akiwa na hamu ya kucheza inabidi adhibitiwe hadi Kombe la Dunia.

Acha ujumbe