Klabu ya Chelsea na Liverpool wanaripotiwa kumtaka mchezaji wa Napoli Khvicha Kvaratskhelia msimu ujao wa joto, lakini winga huyo anaweza kuwagharimu zaidi ya Pauni milioni 86 endapo ataondoka Napoli.

The Evening Standard Chelsea na Liverpool wanamfuatilia kwa karibu Mgeorgia huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye amekuwa moja ya mchezaji mwenye kiwango bora barani Ulaya tangu alipowasili Naples miezi minne iliyopita.
Klabu hiyo ya Italia ililipa Pauni milioni 9 tu ili waweze kumnasa Kvaratskhelia kutoka Dinamo Batumi katika nchi yake, ambako alirejea mwezi Machi baada ya kughairisha mkataba wake na Rubin Kazan huku kukiwa na mzozo wa Urusi na Ukraine.
Vijana wa Luciano Spalletti ndio vinara wa Serie A wakiwa pointi tano mbele na tayari wameshatinga hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa huku kuanza kwao vizuri michuano hii inaweza kuwa historia kwao.

Kvaratskhelia alifurahishwa na kipigo cha 2-0 cha Napoli kwenye Uwanja wa Anfield Jumanne usiku, huku kocha wa Liverpooli Jurgen Klopp akiweka heshima yake baada ya ushindi huo alioupata akiwa nyumbani kwake.
Klopp alimsifia mchezaji huyo akisema kuwa ana kasi, ni mjuzi, anaweza kuingia ndani au nje, hiyo inafanya kuwa ngumu sana huku akisema kuwa beki wake Trent alicheza mchezo mzuri zaidi yake.
Wakala wa mchezaji huyo, Christian Emile, amekiri kuwa hakuna matarajio ya nyota huyo kuhitajika kuhama Januari lakini anahisi faida kubwa ipo kwenye kadi kwa Napoli ikiwa watamuuza.

Emile alimwambia gwiji wa uhamisho Fabrizio Romano: “Kwangu mimi, kama ataendelea kufanya hivi hadi mwisho wa msimu kwa sababu kuna uwezekano wa 0% wa kumuuza Januari, atafikia €100m bila shaka.”

