Kocha wa klabu ya Juventus inayoshiriki ligi kuu nchini Italia Massimiliano Allegri, Ataendelea kusalia kwenye viunga vya Turin kama kocha mkuu wa klabu hiyo licha ya kutupwa nje kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ulaya.allegriKlabu ya Juventus haitashiriki hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa ulaya kwa mara ya kwanza toka mwaka 2013. Na hii imekuja baada ya jana kupoteza mchezo wao wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya klabu ya Benfica na kuwafanya vibibi hao wa Turin kuaga rasmi mashindano hayo wakiwa na alama tatu pekee kwenye michezo mitano.

Juventus walipokea kipigo cha mabao manne kwa matatu kwenye dimba la Estadio Da Luz nchini Ureno. Kupitia kipigo hicho Benfica wamefikisha alama 11 na kua sawa na vinara wa kundi hilo klabu ya PSG ambapo wamepishana tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.allegriKupitia kipigo hicho maneno yameendelea kua mengi juu ya kocha wa klabu hiyo Allegri na mashabiki wa klabu hiyo na kuona ni muda sahihi kocha huyo aiachie klabu, Kwani matokeo yamekua ya sio ya kuridhisha tangu amerudi kwa mara ya pili kwenye timu hiyo.

Lakini kumeonekana hakuna dalili yeyote ya kumtimua kocha Allegri, Kwani rais wa klabu hiyo Andrea Agnelli amesisitiza kocha huyo bado yupo sana klabuni hapo mpaka utakapofika mwisho wa mkataba wake mwaka 2025.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa