Kocha mkuu wa Juventus Massimiliano Allegri ana uhakika kuwa timu yake hii leo “itakuwa sawa” na inaweza kushinda dhidi ya Benfica  huku matumaini yao ya Ligi ya Mabingwa yakiwa yamening’inia baada ya kuanza vibaya.

 

 Allegri Anaamini Wanaweza Kushinda Hii Leo Dhidi ya Benfica.

Huku mechi iliyopita wakipata kipigo cha kushtukiza kutoka kwa Maccabi Haifa na kuwafanya wawe na hali mbaya huku wakiwa na matumaini finyu ya kuvuka na kwenda hatua nyingine inayofuata.

Juventus wameshinda mchezo mmoja tuu kwenye michuano hii ambapo walimfunga Maccabi Haifa wakiwa nyumbani kwao na hii leo wanahitaji ushindi kwa namna yoyote ambapo watakuwa wamebakiza mechi moja watakayomalizia dhidi ya Psg.

Allegri anasema kuwa hana wasiwasi wowote kuelekea mechi hiyo akiwaambia waandishi wa habari: “Kesho, nadhani itakuwa sawa. Ninaweza kuwa nimekosea, lakini ninajiamini”.

 Allegri Anaamini Wanaweza Kushinda Hii Leo Dhidi ya Benfica.

Allegri anasisitiza kusema kuwa bado hawajaondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa, lakini pia bado hawajafuzu kwenye Ligi ya Uropa. Ni pointi sita zimesalia kwenye mechi mbili na hatima yao haitegemei wao pekee, Benfica kwa upande mwingine ndio wamiliki wa hatima yao.

Mchezaji wao Alex Sandro, pia anaunga mkono timu yake na kusema kuwa timu yao bado ya thamani huku akisema kuwa mchezo huo una thamani kubwa kwao, na ushindi pekee ndio unafaa wako hapo kushinda na kucheza mchezo mzuri na amesisitiza kuwa hawawezi kukosea tena.

“Tutaingia uwanjani kudhihirisha thamani yetu. Tunatumai kuwapa Benfica kipigo chao cha kwanza. Nawafahamu, wengine wana nguvu sana, utakuwa mchezo mgumu sana. Kuna wachezaji wanaweza kuleta mabadiliko wakati wowote. “

 Allegri Anaamini Wanaweza Kushinda Hii Leo Dhidi ya Benfica.

Juventus yupo nafasi ya 3 kwenye kundi H huku Benfica akiwa nafasi ya pili na asiposhinda leo hii, mechi inayofuata anacheza dhidi ya Psg.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa