Kiungo wa zamani na aliewahi kua kocha wa muda wa Man United Michael Carrick amechaguliwa kua kocha wa klabu ya Middlesbrough inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Uingereza.carrickGwiji huyo wa zamani wa vilabu vya Tottenham na Man United amepata nafasi ya kua kocha mkuu kwa mara ya kwanza baada ya kupata cheti chake cha ukocha kutoka shirikisho la soka barani ulaya Uefa hapo kabla.

Michael Carrick amewahi kuaminiwa kwa muda mchache ndani ya Man United baada ya kufukuzwa kwa kocha Ole Gunnar Solskjaer na yeye kukabidhiwa timu na kusimamia kwa muda bila kupoteza mchezo hata mmoja na kufanya mashabiki kuanza kuona mwanga kwenye maisha yake ya ukocha kama ataaminiwa na kupewa timu.carrickCarrick anaungana na magwiji wa zamani wa klabu hiyo kuingia kwenye ukocha kama Gary Neville. Paul Scholes, Ole Gunnar Solskjaer, pamoja na Wayne Rooney ambae kwasasa yupo kwenye klabu ya Derby Country.

Kiungo huyo wa zamani wa United na timu ya taifa ya Uingereza alitangazwa usiku wa jana kua kocha mkuu wa klabu hiyo kuchukua nafasi ya kocha aliepita klabuni hapo na matumaini yakiwa ni makubwa kwa kocha huyo kijana.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa