Kocha mkuu wa Manchester City Pep Guardiola amemsifu mchezaji wa Borrusia Dortmund Jude Bellingham na kusema kuwa ni mchezaji maalumu na ana mawazo ya kipekee, wakati City wakijiandaa kuvaana na Dortmund katika mechi ya Ligi ya Mabingwa hii leo.

 

Guardiola: Bellingham Ni Mchezaji Maalumu.

City watakuwa Signal Iduna Park leo hii wakiwa tayari wamejihakikishia nafasi inayofuata katika raundi ya mtoano, huku shukurani zao zikienda kwa  nyota wa zamani wa Dortmund Erling Haaland ambaye amekuwa ni mshambuliaji wa hatari kwasasa Uingereza.

Lakini kufuatia mchezaji huyo wa Kimataifa wa Norway kuondoka katika klabu hiyo ya Bundesliga, sasa timu hiyo imekuwa ikishikiliwa na mchezaji wa Kimataifa wa Uingereza Jude Bellingham anayezidi kujizolea sifa kedekede.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 alikuwa nahodha wa Dortmund katika mashindano ya ndani na Ulaya kwa mara ya kwanza mapema mwezi huu, na sasa Guardiola amemsifu kama “Mchezaji aliyekamilika”.

Guardiola: Bellingham Ni Mchezaji Maalumu.

“Nadhani Dortmund ni mahali pazuri kwa wachezaji wachanga, wenye vipaji, Labda kama Bellingham angeenda kwenye timu ya juu ya ligi kuu asingeweza muda wa kucheza. Bellingham angeenda kwenye timu ya juu ya Ligi Kuu asingepata dakika za kucheza”

Guardiola aliongeza kwa kusema kuwa njia bora kwa mchezaji mchanga kuwa bora ni kucheza, na tayari ni mmoja wa manahodha wao tangu akiwa na miaka 19 ni jambo la kushangaz. Sio tuu kuhusu mabao, yeye pia ni mchezaji mzuri na tayari anaichezea Uingereza akiwa na umri huo na wanajua ubora alionao.

Huku wenyeji wao wakiwa bado wanahitaji matokeo ili kujihakikishia kufuzu, Guardiola anajua kwamba atakabiliwa na mtihani mgumu nchini Ujerumani na anafurahia kikosi chake kucheza mbele ya ukuta maarufu wa timu hiyo kwa mara nyingine tena.

Guardiola: Bellingham Ni Mchezaji Maalumu.

Guardiola alimalizia na kusema kuwa uwanja wao ni mzuri na kila mtu anaujua, hali ya anga, soka la kuvutia wanalocheza, na ana furaha kurejea hapo. Mechi ya kwanza City alivyokuwa nyumbani alishinda kwa mabao 2-1. Je leo hii Dortmund atafanya nini?

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa