Kocha wa zamani wa klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane amezungumza kua ana uwezekano wa kurejea kwenye ukocha hivi karibuni baada ya kuulizwa kuhusiana na kufundisha siku za hivi karibuni.zidane

Kocha huyo pekee aliewahi kubeba taji la ligi ya mabingwa ulaya mara tatu mfululizo akiwa na Real Madrid alifunguka hayo akifanya mahojiano na kituo kimoja baada ya kuulizwa uwezekano wa yeye kurejea kwenye ukocha hivi karibuni.

“Je, Ninakosa suti ya kufundisha? Hapana ninarejea hivi karibuni” Alisema Zidane mchezaji bora wa dunia mwaka 1998.zidaneKocha huyo amekaa pembeni kwa takribani mwaka sasa toka aachane na klabu ya Real Madrid mwaka 2021 baada ya kuipa mafanikio makubwa klabu hiyo katika vipindi tofauti tofaut.

Zidane amekua akihusishwa mara kadhaa kujiunga na klabu ya PSG pamoja na timu ya taifa ya Ufaransa ambayo kwasasa ipo chini ya kocha Deschamps lakini inaonekana kiungo huyo wa zamani wa taifa hilo anapigiwa chapuo kuchukua kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya Ufaransa baada ya michuano ya kombe la dunia.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa