Callum Hudson-Odoi amesema kuwa ana furaha kuichezea Leverkusen kwa mara nyingine tena ambapo yupo klabuni hapo kwa mkopo baada ya kuona hana nafasi katika klabu ya The Blues na kuamua kutimkia Ujerumani.

 

Callum Hudson-Odoi Asema Kuwa Ana Furaha Leverkusen.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 na Muingereza alihamia Leverkusen mwezi Agosti kwa kipindi cha kampeni za msimu wa 2022-23 baada ya kuanza mara 11 tu kwenye Ligi ya Uingereza  chini ya Thomas Tuchel msimu uliopita. Hudson-Odoi tayari ameanza mechi nane kwa Leverkusen katika Bundesliga na Ligi ya Mabingwa, akicheza zaidi kama mshambuliaji wa upande wa kushoto.

Callum amesema kuwa; “Haijalishi ni wapi nilikuwa nikicheza, siku zote nilikuwa nikijaribu kufanya niwezavyo na kuisaidia timu – siku zote hainihusu. Sikuwahi kubishana; niliendelea nayo.”

Hudson-Odoi aliongeza katika mahojiano yake na The Athletic akiseama kuwa maoni yake hayakukusudiwa kama ukosoaji wa Tuchel, lakini zaidi kufadhaika kwa misimu yake michache iliyopita huko Chelsea.

Callum Hudson-Odoi Asema Kuwa Ana Furaha Leverkusen.

Kwa kuwa na wachezaji wengi wazuri kwenye timu, lazima upiganinie nafasi yako na ufanye bidii zaidi, na ilikuwa ngumu lakini lazima uendelee nayo na ufanye kile unachoweza.

Callum anasema kuwa hakuondoka Chelsea kwa kuwa alikuwa hapapendi, lahasha, bali alikuwa akitaka kupata nafasi ya kucheza soka mahali tofauti na Darajani ili ajaribu awezavyo kisha arudi Chelsea baada ya kumalizika kwa mkopo wake.

Callum bado hajafunga katika mechi 10 alizocheza Leverkusen, ingawa amesaidia bao kwenye klabu hiyo. Leverkusen wako pointi moja tu juu ya eneo la kushuka daraja la Bundesliga baada ya kuanza vibaya kwa kampeni ambapo walimtimua kocha wao Gerardo Seoane na kumchukua Xabi Alonso.

Callum Hudson-Odoi Asema Kuwa Ana Furaha Leverkusen.

Bila kujali kiwango chao cha kukatisha tamaa, Callum  ana furaha kucheza soka la kawaida katika ligi kuu ya Ujerumani. Na amesema kuwa licha ya kutokuwa na matokeo mazuri lakini kulingana na uzoefu, yamekuwa mazuri sana na ana furaha kuwepo hapo, anahisi kama yupo nyumbani.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa