Aliyekuwa mchezaji wa Chelsea Hudson Odoi amefichua kwa Daily Mail: Toddy Boehly hakutaka kujumuisha chaguo la kununua na akamwambia: Sikiliza tunataka urudi hapa . Bado upo kwenye rada za Chelsea.

 

Odoi Aongea Kuhusu Alichoambiwa na Toddy

Odoi alisema kuwa “Kuna wachezaji wengi wachanga ambao anajaribu kununua kwa miaka ijayo, ni sehemu kuu ya mradi”

Ikumbukwe kuwa Odoi mpaka sasa yupo kwa mkopo katika klabu ya Bayer leverkusen ya huko Ujerumani ambapo alienda msimu huu wa joto kabla ya dirirsha kubwa kufungwa mwezi Septemba.

Odoi ambaye ana umri wa miaka 22 na anacheza katika eneo la winga amekuwa akipatia wakati mgumu kupata nafasi ya kucheza katika klabu ya Chelsea  baada ya ujio wa Thomas Tuchel ambapo msimu mzima amecheza mechi zisizozidi 15 ambapo hata hizo mechi alizocheza hachezi dakika zote tisini.

 

Odoi Aongea Kuhusu Alichoambiwa na Toddy

Hivyo kutokana na ufinyu huo wa namba Chelsea waliamua kumtoa kwa mkopo kutokana na kuwa na wachezaji wenye ubora wengi wanaocheza katika eneo hilo huku pia akiwa sio chaguo pendwa la aliye kocha huyo. Hivyo baada ya kuondoka kwa Tuchel Odoi anatumaini anaweza kurudi klabuni hapo huku Boss wa timu hiyo  Toddy  Boehly akimwambia kuwa bado anahitajika kikosini hapo.

Bayer Leverkusen katika mechi 7 alizocheza ameshinda mechi 1, ametoa sare mechi 2 huku akipoteza michezo 4 na kwenyee msimamo yupo nafasi ya 15. Matokeo hayo yanayodhihirisha kuwa bado wana hali mbaya kutokana na kuanza kwao vibaya msimu huu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa