Klabu ya Chelsea inafikiria kumtoa kwa mkopo winga wao Hudson Odoi ambaye atapelekwa kwenye klabu ya Bayer Leverkusen, mazungumzo kati ya pande zote mbili yanaendelea vizuri na huenda yakakamilika mwishoni mwa wiki hii.

odoi, Hudson-Odoi kutolewa kwa Mkopo Bayer Leverkusen, Meridianbet

Mchezaji huyo mwenye miaka 21, alipata majeraha mwishoni mwa msimu ulioisha na hata baadaya kupona bado hajamshawishi zaidi kocha wake Thomas Tuchel ambaye ameshauri atolewe kwa mkopo.

odoi, Hudson-Odoi kutolewa kwa Mkopo Bayer Leverkusen, Meridianbet

Timu baadhi za ligi kuu ya Uingereza kama NewCastle United, Leicester City, na Southampton walionekana kumtaka mchezaji huyo.

Taarifa kutoka kwa kaka wa Odoi ambaye pia ni wakala wake Bradley Hudson Odoi alisema kuwa mazungumzo kati yao na Bayer Leverkusen yapo kwenye hali nzuri na muda wowote mchezaji huyo ataondoka Chelsea kwenda kujiunga na timu hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa