Staa wa muziki wa kizazi kipya Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz aibukia mitaa ya Old Trafford yalipo makazi ya timu ya Manchester United.

Staa huyo wa muziki wa kizazi kipya alihudhuria mchezo uliozikutanisha klabu za Manchester United dhidi ya Liverpool ambapo mchezo huo uliisha kwa United kushinda goli mbili kwa moja.

ommy dimpoz, Ommy Dimpoz Uso Kwa Uso na Ronaldo., Meridianbet

Ommy Dimpoz ambae ni shabiki mkubwa wa Manchester United ambae alihudhuria mchezo huo katika dimba la Old Trafford usiku wa jumatatu ameweza kuikamata mitandao tofauti tofauti ya kijamii baada ya kuchapisha picha kwenye mitandao yake ya kijamii akiwa na wachezaji wa klabu hiyo. Ila kubwa zaidi ni picha aliyochapisha akiwa na nyota wa dunia Cristiano Ronaldo ambayo ndo imekua gumzo sana mitandaoni.

Ommy Dimpoz ambae alihudhuria mchezo huo katika usiku wa jumatatu amedai amepata mwaliko rasmi kutoka kwenye klabu kuweza kupiga picha na wachezaji wote wa klabu hiyo. Huku kwa upande mwingne amedai anamsaidia Rais wa nchi Mama Samia Suluhu Hassan kutangaza utalii wa nchi kwani miongoni mwa picha alizopiga na wachezaji wa klabu hiyo mojawapo alishika jezi ya Tanzania yeye na staa wa klabu hiyo Bruno Fernandes.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa