Mchezaji wa klabu ya Leicester city inayoshiriki ligi kuu ya uingereza Wesley Fofana ameendelea kusisitiza juu ya nia yake ya kujiunga na klabu ya Chelsea.

Beki huyo mwenye miaka 21 mzaliwa wa Ufaransa mhitimu wa akademi ya Saint Etienne anatamani kwenda klabu ya Chelsea na kwake anaiona kama klabu ya ndoto zake.

fofana, Wesley Fofana Anaitaka Chelsea., Meridianbet

Chelsea waliamua kumgeukia beki huyo ni baada ya kukosa beki mwingine raia wa Ufaransa Julias Kounde alietimmkia klabu ya Fc Barcelona ya nchini Hispania.

klabu ya Chelsea wamepeleka ofa tofauti tofauti kwa klabu ya Leicester City inayommiliki mchezaji huyo lakini zote zimepigwa chini mpaka ofa ya mwisho ya paundi milioni 70 nayo imepigwa chini. Lakini upande wa mchezaji inaonekana kuhitaji dili hilo litimie ili aweze kujiunga na klabu ya Chelsea.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa