KLABU ya Simba imepanga kufanya balaa kwenye mechi zao tatu watakazocheza kwenye mikoa miwili ya Kanda ya Ziwa, Mwanza na Kagera kwenye mechi za ligi kuu.

Simba wamepanga kuvuna alama tisa kwenye mechi hizo kwa maana kuvuna alama tatu kwenye kila mechi ili kujiweka sawa kwenye mbio za kusaka ubingwa wa msimu huu.

Simba wanazitaka alama tisa (09) Kanda ya Ziwa

Simba wanatarajia kushuka dimbani leo Jumapili kwenye uwanja wa CCM Kirumba kucheza na Geita Gold FC ikiwa ni mechi yao ya kwanza, kisha baada ya siku tatu watakuwa kwenye uwanja wa Kaitaba Bukoba kucheza na Kagera Sugar.

Baada ya hapo watarejea tena Mwanza kucheza na KMC kwenye mchezo ambao utachezwa Desemba 26, KMC wakiwa wenyeji wa mechi hiyo wakitumia faida ya kikanuni ya kucheza nje ya Dar au uwanja uliopo mkoani kwako.

Simba wanazitaka alama tisa (09) Kanda ya Ziwa

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally amesema kuwa: “Tunataka kuondoka huku Kanda ya Ziwa na kurudi nyumbani tukiwa na alama tisa kwa maana tunataka kushinda mechi zote tatu.

“Tutaanza kuwaburuza Geita Gold FC, tunawajua wana timu bora na wachezaji wazuri, lakini alama zao tatu tunazitaka. Baada ya kumalizana na Geita tutawafuata Kagera Sugar kule kwao.

“Walitufunga msimu uliopita, tunakumbuka hilo, lakini awamu hii hawatoweza na baada ya hapo tutarudi kwenye ardhi ya Mwanza kumalizana na KMC. Kimsingi alama zao tatu watu wote hawa tunazihitaji.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa