Simba wazipania pointi tisa (09) ugenini

Uongozi wa klabu ya Simba umeweka wazi kuwa mipango yao ni kuhakikisha wanavuna pointi tisa kwenye michezo mitatu ya ugenini.

Timu hii inatarajia kucheza michezo mitatu ugenini dhidi ya Geita Gold, Kagera Sugar na KMC.

Simba wazipania pointi tisa (09) ugenini

Akizungumzia mipango yao, Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally alisema “Mipango yetu ni kuhakikisha tunazipata pointi zote tisa kwenye michezo hii mitatu ya ugenini.

Simba wazipania pointi tisa (09) ugenini

“Tukianza na Geita Gold tunajua ni timu nzuri ya ushindani hasa inapokuwa kwenye Uwanja wao wa nyumbani lakini sisi tunahitaji kutetea ubingwa hivyo inabidi tupate ushindi kwenye mchezo huu.

“Tunatambua kwamba tuna michezo mitatu ambayo ni migumu ugenini lakini jukumu letu ni kuhakikisha tunapata pointi zote tisa.

Acha ujumbe