Benzema Amesema Hapendezwi Na Taarifa za Mtandaoni

Mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Ufaransa, Karim Benzema alitumia mtandao wa kijamii ujumbe wa kificho akisema “hapendezwi” siku mbili tu kabla ya mchuano wa fainali ya Kombe la Dunia kati ya Ufaransa na Argentina kupigwa.

 

Mshambuliaji huyo alitolewa nje ya michuano ya Kombe la Dunia Qatar 2022 usiku wa kuamkia michuano hiyo kutokana na jeraha la paja alilolipata mazoezini kabla ya michuano hiyo.

Kulikuwa na maoni kwamba mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d’Or anaweza kuunganishwa na kikosi baada ya kupona jeraha na kurejea mazoezini na klabu yake.

Hata hivyo, alipoulizwa kama Benzema anaweza kurejea kwaajili ya mchezo wa fainali hapo kesho, kocha wa Ufaransa Didier Deschamps alisema: “Sitaki kukujibu. Ni swali la kijinga.”


Ripoti zaidi kutoka Uhispania Ijumaa zilidai Benzema hakufurahishwa kurudishwa nyumbani mara ya kwanza na hakukubali maoni ya hivi punde ya Deschamps.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 sasa amechapisha ujumbe wenye utata kwenye mitandao ya kijamii, uliotafsiriwa tu kama “Sipendezwi”, ukiambatana na emoji ya mlipuko.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Lyon, amefunga mabao 37 katika mechi 97 alizoichezea Ufaransa.

Les Bleus wanalenga kuwa timu ya tatu pekee na ya kwanza tangu Brazil mwaka wa 1962  kuhifadhi taji la Kombe la Dunia baada ya kuilaza Morocco 2-0 katika nusu fainali ili kusonga mbele.

Acha ujumbe