Mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara ulipigwa hapo jana katika uwanja wa Chamazi Complex majira ya saa 3:00 usiku kati ya Ihefu dhidi ya Ruvu Shooting.

 

Ihefu Yaibamiza Ruvu Shooting

Mabao ya Ihefu yalitupiwa kimyani katika kipindi cha pili cha mchezo, bada ya kwenda mapumziko milango yote ikiwa migumu kwa pande zote mbili. Ambapo dakika ya 86 Obrey Chirwa aliwanyanyua mashabiki kabla ya Michael wa Ruvu kujifunga bao dakika ya 88.

Ruvu Shooting wametoka kumtangaza kocha mpya Mbwana Makata aliyewahi kuinoa Dodoma Jiji lakini ameanza vibaya na timu hiyo hali ikizidi kuwa mbaya zaidi kwani anashikilia nafasi ya 15 kwenye msimamo.

Ihefu Yaibamiza Ruvu Shooting

Licha ya Ihefu kupata pointi tatu hizo muhimu wamesalia katika nafasi 14 kwenye ligi na kujikusanyia pointi zao 14 hadi sasa huku wakikazana kufanya vizuri waepuke kushuka daraja msimu huu.

Mechi inayofuata ya Ihefu atakipiga dhidi ya Namungo, wakati kwa upande wa Ruvu Shooting yeye atamenyana dhidi ya Mtibwa Sugar.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa