Mechi ya mwisho ya Ligi hapo kesho itakuwa ile ambayo itawakutanisha Ruvu Shooting dhidi ya Ihefu katika uwanja wa Chamazi majira ya saa 3 usiku.

 

Ruvu Shooting Kujiuliza Dhidi ya Ihefu Hapo Kesho

Ruvu ambayo wana hali mbaya mpaka sasa kwenye Ligi kwani wamejikusanyia pointi 11 tu katika mechi zake 15 alizocheza akiwa ameshinda mechi zake 3 sare mbili, vipigo 10 hadi sasa.

Lakini Ihefu wao wapo nafasi ya 14 wakiwa na hali mbaya kama ya vijana wa Makata, wakiwa wameshinda nao mechi zao tatu pekee, sare mbili na kupoteza mechi 10 wakiwa pointi sawa 11 na wenyeji wao.

Kinachowatofautisha hawa wawili ni mabao ya kufunga na kufungwa huku kwa upande wa Ruvu Shooting itakuwa ni mechi ya kwanza ya Ligi ya kocha wao mpya Mbwana Makata baada ya kukabidhiwa timu.

Ruvu Shooting Kujiuliza Dhidi ya Ihefu Hapo Kesho

Mechi tatu za mwisho kukutana Ihefu ameshinda mbili huku vijana wa Mbwana Makata wakishinda mechi moja pekee.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa