MARA baada ya Simba kupangwa katika kundi D la Ligi ya Mabingwa Afrika na timu za Raja Casablanca, Horoya FC na Vipers, mshambuliaji wa timu hiyo Moses Phiri ameliangalia kundi hilo kisha akatamka neno moja tu kuwa ‘Tunatoboa’.

Simba ndio wawakilishi pekee wa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na wanatarajiwa kuanzia ugenini.

Mshambuliaji huyo alisema kuwa, licha ya ubora wa timu ambazo wamepangwa nazo lakini bado anaona nafasi ya wao kufanya vizuri katika kundi lao na kutinga katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Moses Phiri: Simba itakwenda robo fainali CAF

“Ndiyo ni kweli kundi ni gumu lakini kwa upande wetu tuna matarajio mazuri ya kutoboa na kutinga katika hatua ya robo fainali ambayo ndiyo malengo ya timu katika kila msimu kufika robo na kuendelea mbele”.

“Timu ambazo zipo kwenye kundi zote ni nzuri na zina malengo ya kusonga mbele lakini hata sisi sio wanyonge katika michuano hii na tutahakikisha kuwa tunapambania timu ili tuweze kufanikiwa kufika mbali zaidi,” alisema mshambuliaji huyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa