Klabu ya soka ya Simba inajitafuta kimyakimya kuelekea dirisha dogo la mwezi Januari ambapo inaelezwa klabu hiyo imepanga kufanya usajili wa kutisha katika dirisha hilo.
Klabu ya soka Simba imepanga kuingia sokoni kwenye dirisha dogo kwa kishindo huku malengo yao makubwa ni kuhakikisha timu hiyo inakwenda kufanya vizuri kwenye michuano yote ambayo wanashiriki, Lakini mipango mikubwa zaidi wamewekeza kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Afrika.Inaelezwa kua klabu ya Simba imemalizana na mshambuliaji wa kimataifa wa Congo ambaye ilimtafuta kwa muda mrefu Cesar Lobi Manzoki ambaye alikua anaitumikia klabu ya Vipers kabla ya kutimkia klabu ya Dalian Pro ya China.
Wekundu hao wa Msimbazi pia inasemekana wanafatilia kwa karibu huduma ya alitekua mchezaji wao anayekipiga katika klabu ya Al-Ahly kwasasa Luis Jose Miquisonne kutaka kumrejesha klabuni hapo kuongeza nguvu kuelekea hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika.Siku za hivi karibuni Wekundu wa Msimbazi imeonekana kama ipo kwenye mpasuko mkubwa baada ya aliekua mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo Barbara Gonzalez kujiuzulu, Huku ikielezwa pia mwekezaji wa klabu hiyo Mohamed Dewji kusemekana kutaka kujitoa klabuni hapo lakini timu hiyo inaelezwa inapanga kujijenga kwa kiwango kikubwa kupitia dirisha la usajili la mwezi Januari.