Klabu ya Yanga ambayo ipo chini ya kocha mkuu Nasredine Nabi inaendelea na mazoezi kuelekea mchezo wao dhidi ya Polisi Tanzania siku ya Jumamosi.

 

Yanga, Yanga Yaanza Maandalizi Kuelekea Mchezo wa Jumamosi, Meridianbet

Yanga ambao mpaka sasa ndio vinara wa ligi kuu wakiwa wamecheza michezo yao 15 wameshinda michezo 12 sare mbili na wamepoteza mchezo mmoja hadi sasa wakiwa wamejikusanyia pointi zao 38.

Wakati Polisi Tanzania wao wapo nafasi ya mwisho ambayo ni ya 15 wakijishindia mechi zao mbili, wakienda sare tatu na kupoteza michezo yao kumi, na pointi zao 9 kibindoni hadi sasa.

Yanga, Yanga Yaanza Maandalizi Kuelekea Mchezo wa Jumamosi, Meridianbet

Jumamosi ni mchezo mwingine wa mzunguko wa pili huku timu zote zikihitaji kupata alama tatu muhimu ambazo zitamfanya ajiongezee alama. Je Polisi atafanya nini mbele ya bingwa mtetezi?

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa