Kocha mkuu wa Ufaransa Didier Deschamps aliulizwa iwapo Karim Benzema anaweza kurejea Ufaransa kwa ajili ya fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Argentina na akasema kuwa hataki kujibu swali hilo.

 

Benzema Kurejea Kwenye Fainali Jumapili

Benzema alitolewa nje ya michuano hiyo nchini Qatar kutokana na jeraha la paja, lakini imeripotiwa kuwa anaweza kushiriki katika kikosi cha mabingwa watetezi watakapojaribu kuhifadhi taji lao Jumapili.

Les Bleus ilishinda Morocco 2-0 hapo jana na kufanikiwa kuingia fainali ambayo watamenyana dhidi ya Argentina kwenye Uwanja wa Lusail wikendi hii.

Benzema Kurejea Kwenye Fainali Jumapili

Kocha mkuu wa Ufaransa Deschamps alikataa kusema  iwapo mshindi wa Ballon d’Or Benzema anaweza kushiriki fainali baada ya kurejea kwenye mazoezi na Real Madrid akisema kuwa; “Sitaki kabisa kujibu swali hilo, ninaomba msamaha.”

Benzema amecheza mechi 12 pekee akiwa na Madrid msimu huu kutokana na jeraha.

Benzema Kurejea Kwenye Fainali Jumapili

Mabao kutoka kwa Theo Hernandez na Randal Kolo Muani yaliiweka Ufaransa katika fainali nyingine ya Kombe la Dunia

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa