Kiungo wa klabu ya soka ya Simba Sadio Kanoute amefanikiwa kutwa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Novemba ndani ya klabu hiyo akiwapiga chini wenzake.

kiungo huyo ambaye amekua kwenye kiwango bora sana katika klabu hiyo tangu arejee kutoka kwenye majeraha, Kiungo huyo amefanikiwa kua kiungo bora kwa mwezi Novemba kutokana na ubora alioupnesha ndani ya mwezi huu kwenye timu hiyo.kanouteKiungo Sadio Kanoute alikua anagombania tuzo hiyo pamoja na beki wa kulia Shomari Kapombe, pamoja na kiungo Muzamiru Yassin lakini kiungo huyo wa kimataifa wa Mali amefanikiwa kuwabwaga wenzake hao na kubeba tuzo hiyo.

Tuzo hii hutolewa na kampuni ya Emirates Aluminium kila mwezi ndani ya klabu ya Simba ambao ndo wadhamini wakuu wa tuzo hiyo, Lakini pia mashabiki wa Simba hupewa nafasi ya kupigia kura wachezaji wanaowani tuzo hiyo kila mwezi.kanouteKupitia mashabiki wa klabu ya Simba ambao ndio hupiga kura kuchagua mchezaji bora wa mwezi ndani ya klabu hiyo wameidhinisha kiungo Sadio Kanoute kua mchezaji bora wa mwezi Novemba klabuni hapo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa