Klabu ya Ruvu Shooting imemtambulisha Mbwana Makata kuwa Kocha wao mkuu atakayeinoa timu hiyo akirithi mikoba ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Charles  Boniphace Mkwasa.

 

Ruvu Shooting Yamtangaza Kocha Mpya

Makata amechukua nafasi hiyo ya Mkwasa ambaye amejiuzulu kuifundisha Ruvu Shooting baada ya kuwa na mwendelezo mbaya wa matokeo kwenye Ligi kuu ya NBC Tanzania Bara.

Kabla ya kutangazwa kuwa kocha wa timu hiyo, Mbwana Makata alishawahi kuinoa timu ya Dodoma jiji ambayo alipanda nayo Ligi huku akileta ushindani mkubwa kwenye ligi kabla ya kuanza kupata matokeo mabovu yaliyomfanya aondoke klabuni hapo.

Ruvu Shooting Yamtangaza Kocha Mpya

Lakini pia kocha huyo hakuishia kuifundisha Dodoma Jiji peke yake alipita klabu ya Mbeya Kwanza ambayo ilishuka daraja msimu jana baada ya kushindwa kupata matokeo yanayoridhisha.

Makata anaikuta timu hiyo katika nafasi ya 15 kwenye msimamo ikiwa na pointi zake 11 mpaka sasa.

Ruvu Shooting Yamtangaza Kocha Mpya

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa