Josko Gvardiol anasalia na furaha katika RB Leipzig bila  kuharakisha makubaliano ya uhamisho wa awali huku kukiwa na tetesi nyingi zainazongezeka kutoka kwa Real Madrid na Chelsea kumtaka beki huyo.

 

Gvardiol Hana Haraka Kuondoka RB Leipzig

Wakala wa Gvardiol amesema mchezaji huyo ana furaha RB huku akiendelea kung’ara katika Kombe la Dunia akiwa na Croatia, ambao waliishinda Japan kwa mikwaju ya penalti na kutinga robo fainali hapo jana.

Inasemekana kuwa klabu ya Chelsea ilikuwa na ofa ya pauni milioni 77 (€90m)  iliyokataliwa kabla ya kuanza kwa msimu kabla ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 kusaini mkataba mpya na Leipzig.

Madrid nao wanasemekana kuingia katika orodha inayokua ya vilabu bora vya Ulaya vinavyomtaka beki huyo, ingawa Sisic anasisitiza kuwa mteja wake hatalazimishwa kufanya uamuzi wa haraka kuhusu mustakabali wake.

Gvardiol Hana Haraka Kuondoka RB Leipzig

Sisic aliiambia Sky Sport Germany kuwa kuhusu uhamisho unaowezekana msimu wa joto wa 2023, hawana haraka na anaweza kuweka wazi kwamba hakuna makubaliano ya awali na klabu yoyote

“Kwa hakika, vilabu vingi vya juu vimeonyesha nia kwake lakini Josko ana mkataba wa muda mrefu Leipzig, anahisi furaha kabisa akiwa hapa na maendeleo yake ni ya kushangaza kwani RB inacheza vizuri sana chini ya Marco Rose.”

Gvardiol amekuwa mtu anayetegemewa na Zlatko Dalic nchini Qatar, akishika nafasi ya pili kati ya wachezaji wa Croatia kwa kiwango chake na hakuna mchezaji ambaye ameweza kumzidi kwa ubora katika eneo hilo.

Gvardiol Hana Haraka Kuondoka RB Leipzig

Mchezaji mwenzake wa Croatia Borna Barisic anaamini Gvardiol anaonyesha uzoefu ambao unapinga umri wake, akisema ana kila kitu katika soka, na anadhani kuwa anacheza kama mzoefu mwenye mechi 100 kwa timu ya Taifa

Barisic amesema kuwa; “Wakati mwingine ninapomtazama, anapozungumza kabla ya mchezo au mazoezini pia, ni kama ni mchezo fulani usio na shinikizo lolote, kama vile anacheza na marafiki fulani.”

Gvardiol Hana Haraka Kuondoka RB Leipzig

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa