Timu ya Azam FC yenye makazi yake Chamazi jijini Dar es salaam imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kushinda mechi nane mfululizo msimu huu chini ya kocha wake mkuu Kalimangonga Ongala.

 

Azam FC Ndiyo Timu ya Kwanza Kushinda Mechi 8 Mfululizo 2022

 

Azam ilianza kushinda mechi zake hizo baada ya kumtimua aliyekuwa kocha wao Denis Lavagne baada ya kupoteza mechi yake yake dhidi ya KMC kwa mabao 2-1 katika uwanja wa Uhuru.

Baada ya hapo Azam FC ilitua kwenye mikono ya Kally Ongala na mechi yake ya kwanza katika klabu hiyo ilikuwa ni ile ya Simba ambapo aliiadhibu kwa bao 1-0 kupitia kwa mshambuliaji wake Prince Dube na kuondoka na pointi 3.

Azam FC Ndiyo Timu ya Kwanza Kushinda Mechi 8 Mfululizo 2022

Hivyo mpaka kufikia mchezo wa jana waliocheza dhidi ya Polisi Tanzania unakuwa wa nane kushinda mfululizo na kuendelea kusalia katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC wakiwa na pointi zao 35.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa