Karim Benzema Nitastaafia Real Madrid.

Staa wa klabu ya Real Madrid na timu ya Taifa ya Ufaransa Karim Benzema amesema anapanga kustaafia klabuni kwakua hakuna nafasi nyingine ambayo anaiona yeye.karim benzemaStaa huyo mshindi wa tuzo ya Ballon Dor amezungumza hayo katika halfa ya ugawaji wa tuzo hizo jana usiku wakati akiibuka mshindi wa tuzo hiyo pale alipoulizwa na mwandishi wa habari kuhusu hatma yake ndani ya klabu hiyo.

“Nimepanga kustaafu hapa Real Madrid. Hakuna sehemu nyingine ninayoweza kustaafia ndivyo nionavyo mimi” Alisema Karim Benzema.

Staa huyo ambaye anashikilia kiatu cha mfungaji bora wa ligi kuu ya Hispania pamoja na ligi ya mabingwa ulaya tayari amefikisha miaka 14 ndani ya klabu hiyo amepanga kumalizia soka lake kwenye klabu hiyo ambayo amefanikiwa kushinda mataji mbalimbali ndani ya klabu hiyo.karim BENZEMAKarim Benzema anaona klabu hiyo hiyo kama sehemu pekee ya kumalizia soka lake kwasababu ndio klabu kubwa kabisa duniani hivo haoni kama kuna sehemu nyingine atakwenda baada ya Real Madrid ikawa na ukubwa zaidi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.