Perez Sina Taarifa za Mbappe Kuondoka PSG Januari.

Rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez amefunguka kua hakua na taarifa ya mchezaji wa klabu ya PSG kuhama klabu hiyo mwezi Januari.perezWakati wa hafla ya ugawaji wa tuzo za Ballon Dor ambapo Rais huyo alihudhuria katika tuzo hizo zilizofanyika nchini Ufaransa ndipo alipoulizwa kuhusu mchezaji Kylian Mbappe ambae aliripotiwa mapema wiki iliomalizika kutaka kuondoka klabuni hapo ndipo Rais huyo aliposema hajui chochote kuhusu taarifa hizo.

“Sio kwamba nimechoshwa na Mbappe, Ila ukweli ni kua sijaipata hiyo habari. Tayari tulikua na msimu mzuri wa kiangazi kwahiyo hilo sio swali” Alisema Perez wakati akiulizwa kuhusiana na mchezaji huyo.

Lakini wakati huohuo Rais Perez huyo hakuonesha kufuta uwezekano wa kutomsajili mchezaji tena ndani ya klabu ya Real Madrid pale aliposema “Huwezi kujua lolote kuhusu siku za usoni, Lakini wachezaji wa Real Madrid wanaendelea vyema katika maeneo ya mbele. Rodrygo, Vinicius bado wana maisha ya kufanikiwa. Wote wanaweza kushinda Ballon Dor siku moja”perezMbappe ambaye alikaribia kusajiliwa na klabu ya Real Madrid majira ya joto yaliyopita na kubadili mawazo na kuamua kubaki ndani ya PSG jambo lililowafanya mashabiki wengi wa klabu ya Real Madrid kuchukizwa na uamuzi huo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.