Staa wa klabu ya Real Madrid Karim Benzema kurejea leo dimbani dhidi ya klabu ya Osasuna katika dimba la Santiago Bernabeu baada ya kukosekana kwenye michezo kadhaa.

Karim Benzema ambaye amekua na msimu bora sana kwa mwaka 2021/22 na kufanikiwa kumaliza kama mfungaji bora wa ligi kuu nchini Hispania na ligi ya mabingwa ulaya na kufanikiwa kuisaidia klabu hiyo kubeba mataji yote mawili aliyomaliza kama mfungaji bora.

karim benzemaStaa huyo raia wa Ufaransa alipata majeraha katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya klabu ya Celtic kutoka nchini Uskochi na kukosa michezo mitatu mmoja ukiwa wa ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya Rb Leipzig na miwili ikiwa ya ligi kuu nchini Hispania ukiwemo mchezo wa Madrid dabi dhidi ya mahasimu wao klabu ya Athletico de Madrid.

Karim Benzema anarejea leo katika mchezo wa ligi kuu nchini humo dhidi ya klabu ya Osasuna ikiwa ni baada ya kukabidhiwa tuzo zake za mfungaji bora wa ligi kuu nchini humo na mchezaji bora wa ligi hiyo katikati ya wiki.

karim benzemaMshambuliaji huyo ambaye amesema anatazamia kufanya makubwa zaidi msimu huu zaidi ya mwaka jana huku kukiwa na upinzani mkubwa katika ligi hiyo msimu huu baada ya ujio wa mshambuliaji hatari Roberto Lewandowski kuhamia klabu ya Barcelona.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa