Salim Abdallah 'Try Again' Azungumzia Usajili Simba | Wanasimba Wakae Mkao wa Kula

BAADA ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa leo Disemba 16, 2022 ikiwa ni kwa muda wa siku 30 mpaka pale Januari 15, 2023, hatimaye sasa uongozi wa Simba umevunja ukimya kuhusu tetesi za usajili Simba kwa wachezaji wanaohusishwa na timu hiyo.

 

Usajili simba

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC Salim Abdallah Muhene maarufu kama Try Again, amesema kwamba wanasimba wakae kwa kutulia, usajili Simba dirisha hili DOGO.

“Tutafanya usajili kwenye maeneo machache ya kuongezea kulingana na ripoti ya wataalam wetu” Salim Abdallah.

Kuhusu tetesi za usajili Simba wa Manzok na Saidoo kuhitajika na KLABU hiyo alisema kuwa wataalam wa timu ndiyo wanafanya usajili hivyo wanasimba watulie.

 

usajili Simba

“Tuseme kwamba kazi ya kusajili ni ya wataalamu kwahiyo naomba hili tuwaachie wao, Caser Manzoki, Adebayor na wengine wanaotajwa wote ni wachezaji wazuri, wanasimba watafurahi taarifa njema zinakuja”

“Watu wapuuze taarifa za mtaani, Luis Miquissone ni mchezaji halali wa timu ya Al Ahly ya Misri, kuhusu hilo wanasimba watapata taarifa halisi kwenye akaunti zetu” -Salim Abdallah

 

usajili Simba

Acha ujumbe