Makata ataja maeneo matatu ya maboresho Ruvu

Kocha Mkuu wa kikosi cha Ruvu Shooting, Mbwana Makata amefunguka kuwa kuna haja ya kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho katika dirisha hili dogo.

Dirisha dogo la usajili limefunguliwa juzi alhamis kwa ajili ya klabu za ligi kuu, Championship, ligi daraja la kwanza, na ligi ya wanawake.

Aidha jana ijumaa Ruvu Shooting walicheza mechi yao ya kwanza kwenye mzunguko wa pili dhidi ya Ihefu ambapo walipoteza kwa mabao 2-0.

Makata ataja maeneo matatu ya maboresho Ruvu

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Makata alisema “Kuna baadhi ya makosa madogo ya kiufundi yamepelekea kupoteza mchezo.

“Kuna wachezaji nane wa kikosi cha kwanza wote wameenda kwenye kozi hivyo ambao tunawatumia baadhi siyo nafasi zao ambazo wanacheza.

“Nimeongea na viongozi kuwa tunahitaji kuboresha zaidi eneo la ulinzi, kiungo pamoja na ushambuliaji kwa ajili ya kuisaidia timu.”

Acha ujumbe