Kocha Msaidizi wa Ihefu, Zuber Katwila amefurahishwa na ushindi kwenye mchezo wa kwanza mzunguko wa pili dhidi ya Ruvu Shooting.

Ihefu walipata ushindi huo wa mabao 2-0 jana ijumaa kwenye mchezo wa ligi kuu uliopigwa katika Uwanja wa Azam Complex.

Katwila afurahia ushindi

Akizungumzia hali ya kikosi chake, Katwila alisema “Kwanza tunamshukuru Mungu kwa kupata pointi tatu kwenye mchezo wetu wa kwanza katika mzunguko wa pili.

“Nilivyoingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo sikuongea maneno mengi bali niliwaambia tukiendelea kujiachia tutapoteza mchezo ila tukitumia nafasi tutaondoka na ushindi hivyo ninawapongeza kwa ushindi“.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa