Kikosi cha Pan African kesho jumapili kinatarajia kumenyana na Mbeya Kwanza kwenye Uwanja wa Uhuru ukiwa ni mchezo wa ligi ya Championship.

Akizungumzia maandalizi yao, Ofisa Habari wa Pan African, Leen Essau amesema kuwa maandalizi yao kiufundi yamekamilika kuelekea kwenye mchezo huo.

“Maandalizi kuelekea mchezo wa kesho yamekamilika kiufundi baada ya mazoezi ya mwisho ambayo yalisimamiwa na kocha Mkuu, Iddy Cheche.

Wawili Pan kuikosa Mbeya Kwanza

“Tutawakosa wachezaji wawili kwenye kikosi cha kwanza ambao ni Alex Peter ambaye ni mgonjwa na Hassan Njete ambaye anatumikia adhabu ya Bodi ya Ligi.

“Kocha amefanya mabadiliko kadhaa hivyo mchezo wa kesho utakuwa na mabadiliko na tuna imani tutapata matokeo mazuri.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa