Gwiji wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa mwenye asili ya Argentina David Trezeguet amefunga kua fainali ya kesho kati ya Ufaransa na Ufaransa imekua ngumu sana kwake binafsi kwakua anahitaji Lionel Messi abebe taji hilo.

Gwiji huyo mshindi wa kombe la dunia mwaka 1998 akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa anafikiri nahodha wa Argentina Lionel Messi anastahili kubeba taji hilo kuliko staa wa timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe.trezeguetGwiji Trezeguet amesema anasumbuliwa na hisia kuelekea katika mchezo huo kwani yeye kama Mfaransa anajua wanataka kutetea taji hilo libaki mikononi mwao, Lakini hisia zake zinamtuma kua Lionel Messi anastahili zaidi kwakua anajua hili litakua kombe lake la dunia la mwisho.

David Trezeguet ambaye yeye ataweza kushangilia ushindi wowote utakaopatikana katika mchezo wa kesho, Lakini anajua wazi kua kuna upande wachezaji wengi watavunjika mioyo sana na kuumia baada ya kupoteza fainali hiyo.trezeguetTimu ya taifa ya Ufaransa itakipiga dhidi ya Argentina kesho katika mchezo wa fainali ya kombe la dunia utakaopigwa katika dimba la Lusail, Mchezo huo utaamua ni nani kati ya timu hizo atakua na nafasi ya kuongeza taji la tatu kwenye kabati lake kwani wote wana mataji mawili ya kombe la dunia.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa