Mgunda: Maandaliz Yamekamilika Kuwakabili Geita

Kocha wa klabu ya Simba Juma Mgunda amesema kua klabu hiyo imekamilisha maandalizi yake kuelekea mchezo wao wa kwanza kwenye ungwe ya pili ya ligi ya NBC.

Klabu ya Simba ambayo kwasasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC wakiwa na alama 34, Huku vinara klabu ya Yanga wakiwa na alama 38 hivo mabingwa hao wa zamani wa ligi hiyo wana nafasi ya kupanda juu ya msimamo endapo watashinda mchezo wao wa kesho.mgundaKocha Mgunda ameeleza wazi kua “Maandalizi ya kuwakabili yamekamilika kuelekea mchezo wa kesho, Na wachezaji wapo kwenye hali nzuri, Tunawaheshimu Geita na tunatarajia kupata ushindani mkubwa katika mchezo huo lakini tupo tayari kuwakabili

Simba wao wameingia jijini mwanza toka siku ya Alhamisi kwajili ya kujiandaa na mchezo huo dhidi ya Geita Gold miongoni mwa timu ngumu ndani ya ligi kuu ya NBC, Lakini wekundu wa msimbazi wao mipango yao ni kuchukua alama tatu muhimu.mgundaKikosi cha Simba chini ya kocha Juma Mgunda kina nafasi ya kuongoza kukaa nafasi ya pili kama watashinda mchezo huo kwani watafanikiwa kufikisha alama 37, Ambapo klabu ya Azam inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 36 baada ya kusuluhu jana mabao mawili kwa mawili dhidi ya klabu ya Kagera Sugar.

Acha ujumbe