Wenger: Kiwango cha Messi kinaonesha Mageuzi ya Mpira

Kocha wa zamani wa klabu ya Arsene Wenger amesema kiwango kikubwa ambacho anaonesha kwenye michuano ya kombe la dunia kinaonesha mageuzi ya mpira wa miguu.

Kumekua na namba kubwa ya wachezaji wenye umri mkubwa kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka huu ambao wameweza kufanya vizuri na mataifa yao ikiwemo Lionel Messi aliyeiongoza timu yake kufika fainali.wengerWachezaji kama Luca Modric mwenye umri wa miaka 37 ameonekana kufanya vizuri kwenye michuano hii, Pia staa wa timu ya taifa ya Ufaransa Olivier Giroud ambaye ana umri wa miaka 35 ameshuhudiwa akivunja rekodi ya ufungaji bora ya muda wote ya timu ya taifa ya Ufaransa katika umri huo.

Kocha Wenger anasema wakati anaiongoza Arsenal dhidi ya Barcelona kwenye fainali ya ligi ya mabingwa ulaya mwaka 2006 Messi alishaanza kucheza na mpaka leo anacheza ni miaka 16 sasa na hii inaonesha mageuzi ya mpira.wengerKocha Arsene Wenger aliendelea kusisitiza kua teknolojia imewasaidia sana wachezaji kuendelea kuonesha ubora mkubwa licha ya kua na umri mkubwa, Kwani wachezaji kama Messi,Giroud, na Modric ni baadhi ya wachezaji wakongwe walioonesha ubora mkubwa kwenye michuano hiyo.

Acha ujumbe