Wenger Amsifu Van Gaal

Kocha wa zamani wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger ambae kwasasa ni kiungozi wa jopo la utafiti ndani ya Fifa amemsifu kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi Louis Van Gaal.

Wenger amemsifu Van Gaal kwa kua kocha anaejua kucheza kamari wakati ambao inahitajika yaani akimaanisha kocha huyo wa timu ya taifa ya Uholanzi anajua kubadilika kutokana na wakati sahihi.wengerKocha wa timu ya taifa ya Uholanzi  Louis Van Gaal amekua akipokea shutuma kua timu yake inachosha na haivutii kuitazama kutoka kwa baadhi ya wachambuzi na mashabiki mbalimbali wa soka. Huku kocha wa zamani wa Arsenal yeye akiwa haamini kama Van Gaal havutii bali anaamini anajua kubadilika kwa wakati sahihi.

Uholanzi imefanikiwa kumaliza kama kiongozi kwenye kundi A na kufanikiwa kuifunga Marekani kwenye hatua ya 16 bora kwa mabao matatu kwa moja na kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la dunia.

Kocha huyo huyo wa zamani wa Barcelona,Bayern Munich, na Manchester United amewahi kuifikisha timu hiyo hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil na kufanikiwa kua mshindi wa tatu.wengerWenger haamini kama Van Gaal ana mbinu za kizamani zaidi anaamini kua kocha huyo ameamua kubadilika kutokana na wakati kwakua kocha huyo ni mtu aliefanya mambo makubwa kwenye soka hivo anajua anafanya nn kwasasa.

Kikosi cha Uholanzi kimekua kikicheza mchezo kumiliki mpira kwa muda mrefu na kushambulia kutokana na falsafa ya mpira wao lakini mwaka huu inaonekana wanacheza kwa kujilinda muda mrefu kitu kinachofanya Van Gaal kukosolewa vikali.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.